Mwangeza, Tanzania – Februari 2025: Wanakijiji wa kabila la Hadzabe kutoka kitongoji cha Kipamba, kijiji cha Munguli, kata ya Mwangeza, wamepata fursa ya kuelimishwa kuhusu haki za makundi mbalimbali ya binadamu kupitia kampeni ya msaada wa kisheria. Elimu hii imelenga kuwawezesha wanakijiji hao kutambua haki zao msingi na kujua namna ya kuzitetea katika mazingira yao ya kiutamaduni na kijamii.
Lengo la Elimu ya Msaada wa Kisheria kwa Makundi Maalumu Katika jamii za makundi maalumu kama Hadzabe, changamoto kubwa zinajitokeza kutokana na mifumo ya kiasili, ukosefu wa taarifa sahihi, na ubaguzi wa kijamii unaoweza kuathiri upatikanaji wa haki zao za kisheria. Kwa kutambua umuhimu wa kundi hili katika historia na tamaduni za Tanzania, watoa elimu walibainisha kuwa kampeni hiyo imelenga kupunguza migogoro ya ardhi, ndoa, urithi, na matumizi ya rasilimali za asili.
#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @dr_philip_isdor_mpango @biteko
@katibanasheria_ @profkabudipjam @victoria.mwanziva @TanganyikaLaw
https://x.com/MsLACampaign/status/1887853294116286558