Skip to main content

BRELA YAUNGANA NA MSLAC KUTOA HUDUMA ZA KISHERIA KWA USAJILI WA BIASHARA NA MAKAMPUNI

Submitted by admin on 18 June 2025

Katika kuunga mkono juhudi za Mama Samia kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria (MSLAC), BRELA imejitokeza rasmi kushiriki kwa kutoa elimu na huduma za kisheria bure kwa wananchi kuhusu usajili wa makampuni, majina ya biashara, na masuala mengine ya kisheria ya uendeshaji biashara.

Kupitia ushirikiano huu, wananchi wengi zaidi wataweza kupata uelewa sahihi wa mchakato wa usajili na haki zao kisheria bila gharama. Hii ni hatua kubwa katika kuhakikisha fursa za kibiashara na maendeleo zinapatikana kwa wote!

🔵 Fuatilia video hii ujifunze zaidi kuhusu huduma zinazotolewa!

🔵 MSLAC na BRELA wanakupelekea msaada wa kisheria hadi mtaani kwako!

#MSLAC #BRELA #MamaSamia #MsaadaWaKisheria #BiasharaTanzania #ElimuYaSheria #TanzaniaInajengwa