Skip to main content

DKT. NDUMBARO ASIKILIZA NA KUTATUA MIGOGORO NDANI YA BANDA LA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA – SABASABA

Submitted by admin on 11 July 2025

Katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba 2025), Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, ameendelea kuonyesha dhamira ya dhati ya kusogeza huduma za kisheria karibu na wananchi kwa kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi papo kwa papo.

Katika video hii, utaona jinsi wananchi walivyopata nafasi ya kueleza changamoto zao za kisheria moja kwa moja kwa Waziri, huku wakipata msaada wa kisheria na maelekezo ya kina kutoka kwa wataalamu waliopo kwenye banda hilo.

Tazama na ujifunze namna Serikali inavyoweka mbele ustawi wa wananchi kupitia utatuzi wa migogoro kwa wakati na kwa haki.

📍 Banda la Wizara ya Katiba na Sheria – Sabasaba 2025

📌 Huduma za msaada wa kisheria bure kwa wananchi

🎯 Haki kwa wakati, bila upendeleo!

#Sabasaba2025 #KatibaNaSheria #DktNdumbaro #MsaadaWaKisheria #MaoneshoYaBiashara