Wananchi wa Arusha waliokuwa kwenye mgogoro wa ardhi ya mirathi kwa zaidi ya miaka 10 hatimaye wamepata suluhu ya kudumu kupitia huduma ya msaada wa kisheria ya Mama Samia – MSLAC. Mgogoro huo ulitokana na msimamizi wa mirathi kuuza eneo la urithi kinyume na makubaliano ya familia.
Baada ya malalamiko ya muda mrefu, wahusika walikimbilia kwa wanasheria wa MSLAC ambao waliwasikiliza, wakatoa ushauri wa kitaalamu na hatimaye wakafanikisha ufumbuzi wa amani bila ugomvi wowote.
Kila upande umeridhika na maamuzi yaliyotolewa – wameshuhudia haki ikitendeka na kuenziwa.
Tazama ushuhuda wa walionufaika na jitihada hizi za kihistoria. MSLAC inaendelea kuandika historia ya haki kwa vitendo!
#MSLAC #MamaSamia #HakiKwaWote #Arusha #MgogoroWaArdhi #MsaadaWaKisheria #LegalAidTanzania