Katika Kongamano la Msaada wa Kisheria la Mwaka 2025 linalofanyika jijini Arusha, wataalamu mbalimbali wa sheria, TEHAMA, na maendeleo ya jamii wanajadili kwa kina nafasi ya ubunifu na matumizi ya teknolojia katika kupanua huduma za msaada wa kisheria.
Mjadala huu unagusa masuala ya mifumo ya kidijitali, majukwaa ya mtandaoni, programu za simu, na suluhisho nyingine bunifu zinazolenga kuwafikia wananchi waishio maeneo ya mbali, wasioweza kumudu gharama au waliokosa taarifa za msingi kuhusu haki zao.
Fuatilia mjadala huu wa kipekee na ujifunze jinsi Tanzania inavyosonga mbele katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wote, bila kujali mahali au uwezo wa mtu.
#MsaadaWaKisheria2025 #UbunifuNaTeknolojia #HakiKwaWote #KongamanoArusha #DigitalJustice #AccessToJustice #MSLAC #KATIBANASHERIA