Katika tukio la kihistoria lililofanyika Songea, Mkoa wa Ruvuma, maelfu ya wananchi wameguswa na nuru ya haki kupitia *Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC)*. Kwa mara ya kwanza, wananchi wameshuhudia haki ikiwafuata mashinani – kwenye vijiji, mitaa na kata zao.
Kampeni hii imebadilisha maisha ya wengi kwa elimu ya sheria, msaada wa kisheria bila malipo, usuluhishi wa migogoro ya ardhi, ndoa, urithi, ajira, na ulinzi dhidi ya ukatili wa kijinsia. Wananchi wengi wameeleza kwa hisia kuwa kampeni hii *“ni ibada”*, siyo huduma ya kawaida bali ni sadaka ya haki na utu kwa Watanzania.
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria, ameongoza mafunzo na uhamasishaji huu kwa viongozi wa mashinani zaidi ya 2,200, huku akieleza kuwa dhamira ya Rais Samia ni kuhakikisha haki inapatikana bila vikwazo.
📌 Tazama video hii ujionee jinsi serikali ya awamu ya sita inavyoweka utu na haki mbele.
💬 Tuambie kwenye comments: Kampeni hii imekugusa vipi wewe au jamii yako?
🔔 Usisahau ku-like, kushare na kusubscribe kwa taarifa zaidi za haki, sheria na maendeleo ya wananchi.
#msaadawakisheria #mslac #MamaSamiaAnasikiliza #HakiKwaWote #LegalAid #Tanzania2025 #Songea #DktNdumbaro #KatibaNaSheria