Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) imeendesha semina kwa watendaji zaidi ya 600 wa kata na mitaa ya Manispaa ya Songea. Lengo ni kuwajengea uwezo wa kutatua migogoro kwa njia mbadala, kuelewa sheria za nchi, kutekeleza majukumu kwa uwajibikaji, na kuimarisha utawala bora katika ngazi ya jamii.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, amesema watendaji hao sasa wanakuwa mabalozi wa haki, wanaopaswa kusuluhisha migogoro badala ya kuichochea.
#MSLAC2025 #MsaadaWaKisheria #DamasNdumbaro #SongeaLive #ElimuYaSheria #MabaloziWaMtaa #UtawalaBora #Uchaguzi2025 #MamaSamiaKwaWote #SongeaYaMaendeleo #RuvumaLive #HakiKwaWote #SheriaNiMsingi #ViongoziNgaziYaMsingi