Katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, amepokea zaidi ya malalamiko 1,900 kutoka kwa wananchi waliomiminika kwenye Banda la Katiba na Sheria kutafuta msaada wa kisheria.
Wananchi walieleza changamoto zao mbalimbali zikiwemo migogoro ya ardhi, mirathi, ndoa, ajira na haki nyingine za msingi. Dkt. Ndumbaro alisikiliza kwa makini na kutoa maelekezo ya haraka huku akisisitiza dhamira ya Serikali kuhakikisha haki inapatikana kwa wote bila upendeleo.
🎯 Hili ni tukio linaloonyesha namna Serikali inavyowakaribia wananchi moja kwa moja
📍 Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam
👥 Huduma ya msaada wa kisheria kwa vitendo
📌 Ushuhuda wa wananchi walioguswa na msaada huu wa moja kwa moja
Tazama video hii ujionee mwenyewe hatua za kweli zinazochukuliwa katika kuhakikisha haki inatendeka!
#Sabasaba2025 #DktNdumbaro #MsaadaWaKisheria #HakiKwaWote #KatibaNaSheria #MaonyeshoYaSabasaba #WizaraYaKatibaNaSheria