/
10 July 2025 /
0 Comments
JULY 7, 2025 GLOBAL TV ON LINE ILITOA TAARIFA HII
"MIAKA 20+ KWENYE NDOA - AFUKUZWA NYUMBA YAKE - ANAISHI KIBARAZANI - MUME AMUOLEA MKE MPYA AISHI KIBARAZANI
Mnamo jioni ya Julai 8, 2025, timu ya maafisa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria ikijumuisha Wakili Msomi Moses Matiko, Michael na Afisa dawati la masada wa kijinsia Omary, ilikutana na mwanamke mmoja eneo la Kimara aliyekuwa akisakwa na Afisa wa Wizara ya katika na sheria kiting cha Masada wa Kisheria MSALAC Edith kutoka banda la Wizara kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba). Hili lilifuatia video fupi ya mama huyo kusambaa mitandaoni, akiwasilisha malalamiko yake kuhusu mgogoro wa kifamilia na kutafuta msaada wa kisheria kutoka serikalini.
Historia ya Kesi kama ilivyo ripotiwa:
Mama huyo alifunga ndoa mbili halali — ya kanisani na ile ya bomani — na mume ambaye kwa sasa ni mzazi mwenziwe. Walijaliwa kupata watoto watatu wenye umri wa miaka 11, 7 na 5.
Mgogoro wao ulianza rasmi baada ya mama huyo kudai kumfumania mumewe akiwa na msichana wa kazi, kitendo kilichopelekea kufungua mashitaka mahakamani.
Kwa mujibu wa hukumu iliyosomwa na kufanyiwa uchambuzi wa kisheria na timu ya Wizara ya Katibu na sherry kitengo cha MSLAC:
- Ndoa yao tayari ilikuwa imevunjika rasmi miaka miwili iliyopita kwa mujibu wa sheria.
- Mahakama iliamua mgawanyo wa mali na usimamizi wa watoto kama ifuatavyo: Ndoa ivunjwe rasmi. Watoto watatu wakae chini ya uangalizi wa baba. Nyumba ya familia ibaki kwa baba. Mama apewe viwanja viwili na gari kama sehemu ya mali waliyoichuma pamoja.
Ushirikiano wa Wizara:
Wizara, kupitia timu yake ya wataalamu waliokwenda kumaliza mgogoro wa muda mrefu kule Mbezi Msumi, ilipokea taarifa hiyo kwa uharaka na kuchukua hatua ya haraka kumsikiliza mama huyo na kumthibitishia hatua zilizochukuliwa kisheria. Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikisha haki inapatikana na maamuzi ya mahakama yanaeleweka kwa walengwa na kwa uwazi huku ikizingatia utu na weledi. Wataalamu hala wanakutana Julai 10 na pande zote mbili Mume na Mke na kuliendesha tena shauri hili kwa Amani utu na upendo
Maoni ya Kitaalamu kutoka kwa wanasheria:
Kesi hii ni mfano halisi wa changamoto za baada ya talaka zinazowakumba wanawake wengi, hasa pale ambapo uelewa wa maamuzi ya mahakama unakuwa hafifu. Pia inaonyesha umuhimu wa usaidizi wa kisheria kwa wananchi kuelewa haki zao, majukumu yao na hatua wanazopaswa kuchukua katika mazingira ya mgogoro.
WITO KWA JAMII:
Wananchi wanaaswa kutumia fursa za msaada wa kisheria zinazotolewa na serikali kupitia kampeni kama MSLAC (Mama Samia Legal Aid Campaign) ili kupata mwongozo wa kisheria kabla ya kuchukua hatua yoyote inayoweza kuwa na athari kubwa kwa familia, watoto na mali walizochuma pamoja.
Wizara inaendelea kutoa msaada huo katika maonesho ya Sabasaba na kupitia ofisi zake kote nchini.