Skip to main content

MBAGARA YAWAKA MOTO WA HAKI: MSLAC NA TAASISI MBALIMBALI WAENDELEA KUTOA HUDUMA ZA KISHERIA BURE..!

Submitted by admin on 23 June 2025

Mbagara, viwanja vya Maturubai vimewaka moto wa haki! Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kisheria imefika kwa wananchi kutoa msaada wa kisheria na elimu juu ya haki zao za msingi. Wananchi wamejitokeza kwa wingi kupata huduma za bure ikiwemo ushauri wa kisheria, uandishi wa wosia, masuala ya ndoa, ardhi, ajira, mirathi, pamoja na njia mbadala za utatuzi wa migogoro.

Ni muda wa kulinda haki, kuelimika na kushiriki katika ujenzi wa jamii inayozingatia utawala wa sheria. Tazama video hii ujionee jinsi wananchi wanavyonufaika, na ujifunze mengi kuhusu haki zako!

#MSLAC #HudumaYaKisheria #MbagaraMaturubai #HakiKwaWote #SioNdotoTena**