MSLAC (Mama Samia Legal Aid Campaign) yaendelea na dhamira yake ya kuwafikia wananchi moja kwa moja! Safari hii, imewafikia wafanyabiashara wa masoko mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwapa elimu ya kisheria kuhusu haki zao, wajibu wao, mikataba ya kibiashara, uandishi wa wosia, na namna ya kushughulikia migogoro ya kisheria bila kutumia nguvu.
Katika video hii, utaona jinsi wananchi wanavyopokea elimu hiyo kwa furaha, wakieleza namna ilivyokuwa hitaji la muda mrefu. Kampeni hii ni sehemu ya maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha haki inapatikana kwa wote – bila ubaguzi, bila gharama.
💬 Tazama, like, comment na share ili ujumbe huu uwafikie Watanzania wengi zaidi!
📌 #MSLAC #MsaadaWaKisheria #MamaSamia #ElimuYaSheria #TanzaniaYaHaki #SioNdotoTena