Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeungana rasmi na Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
Kupitia ushirikiano huu, wananchi sasa wanapata fursa ya:
⚖️ Kupata ushauri wa kisheria moja kwa moja kutoka kwa waendesha mashtaka
⚖️ Kujifunza haki zao kisheria kuhusu masuala ya jinai, ardhi, ndoa, ajira, na urithi
⚖️ Kupata msaada wa haraka na wa kitaalamu bila gharama
⚖️ Kujua namna ya kuwasilisha malalamiko yao kisheria kwa njia salama na sahihi
Hii ni hatua inayodhihirisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati na kwa wote.
Tazama video hii ujionee mafanikio ya ushirikiano huu na msisitizo wa wananchi juu ya umuhimu wa huduma endelevu za msaada wa kisheria.
LIKE 👍🏽 | SHARE 📲 | SUBSCRIBE 🔔 kwa taarifa zaidi kuhusu kampeni hii ya kitaifa.
#MSLAC #MsaadaWaKisheria #OfisiYaMashtaka #DarEsSalaam #HakiKwaWote #SamiaSuluhu #SioNdotoTena