Katika Kongamano la Msaada wa Kisheria la Mwaka 2025 linaloendelea jijini Arusha, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ametoa Wito juu ya wajibu wa wanasheria katika kuhakikisha haki inapatikana kwa kila Mtanzania, hasa wale wa makundi yaliyoko pembezoni.
Akihutubia washiriki wa kongamano hilo, Wakili Mwabukusi amesema:
"Huduma ya msaada wa kisheria haipaswi kuwa jambo la hiari, bali ni wajibu wa kitaifa. Wanasheria tuna nafasi ya kipekee ya kusimama upande wa wanyonge na kuwa daraja lao la kufikia haki.” Amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria, pamoja na wadau mbalimbali wanaojitoa kwa moyo mmoja katika kueneza elimu ya sheria na kutoa msaada wa kisheria katika jamii.
#KongamanoLaMsaadaWaKisheria2025
#TLS #BonifaceMwabukusi #MsaadaWaKisheria #HakiKwaWote #LegalAid2025 #KatibaNaSheria #AccessToJustice #mslac #katibanasheria #sisinitanzania