Skip to main content

TAWLA WAUNGA MKONO JUHUDI ZA MSLAC , JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA VIWANJA VYA MBAGARA MATURUBAI

Submitted by admin on 22 June 2025

TAWLA (Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania) wameungana na Kampeni ya Mama Samia ya Huduma na Msaada wa Kisheria (MSLAC) katika viwanja vya Mbagala Maturubai, jijini Dar es Salaam, kutoa msaada wa bure wa kisheria kwa wananchi.

Katika tukio hili, wananchi wamepata nafasi ya kuelimishwa kuhusu haki zao za kisheria, kuandika wosia, kutatua migogoro ya ardhi, ndoa, ajira, na masuala ya ukatili wa kijinsia. TAWLA wameonesha dhamira ya dhati kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki kwa wakati na kwa njia rafiki.

\#MSLAC #TAWLA #HudumaYaKisheria #MamaSamia #MbagalaMaturubai #HakiKwaWote #SioNdotoTena