Skip to main content

VIONGOZI SONGEA NA MADABA KUPATIWA ELIMU YA UTATUZI WA MIGOGORO SEKTA YA SHERIA

Submitted by admin on 7 May 2025

Wizara ya Katiba na Sheria imeandaa semina itakayotoa Elimu ya utatuzi wa Migogoro  kwa viongozi wa kada ya chini wa Manispaa ya Songea Mjini na wa Wilaya ya Madaba.Image

Akizungumza na Timu ya utoaji wa Elimu hiyo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa ili kumaliza migogoro mbalimbali ya kisheria inayoibuka na ile iliyoibuliwa na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ni vyema kuwapatia elimu viongozi hao ili wakabiliane nayo kuanzia ngazi za chini.

Image

Aidha Mhe. Dkt Ndumbaro amesema mbali ya utatuzi wa Migogoro pia viongozi hao wapatiwe elimu ya uraia na Utawala bora, Elimu ya Ukatili wa Kijinsia na Elimu kuhusu Uchaguzi Mkuu.

Image