Skip to main content

WAFUNGWA 28,137 WANUFAIKA NA MSAADA WA KISHERIA WA MAMA SAMIA

Submitted by admin on 17 June 2025

"Tumekwenda mpaka kwenye Magereza, tumetoa msaada wa kisheria kwa wafungwa 28,137 na leo Mhe. Mgeni rasmi (Waziri Mkuu wa Tanzani) tutakuomba ukabidhi vifaa kwaajili ya magereza, vifaa vya TEHAMA ambavyo vitafanya wafungwa na mahabusu waweze kusikiliza na kuendesha kesi zao wakiwa Magereza hivyo kupunguza gharama za usafiri kwenda Magereza na kurudi, kupunguza kuahirishwa kwa kesi kutokana na kukosekana kwa usafiri lakini pia kufanya Magereza yawe sehemu salama zaidi."- Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya msaada wa kisheria Dar Es salaam leo Jumatatu Juni 16, 2025.