Wizara ya Katiba na Sheria imehitimisha ushiriki wake katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) kwa mafanikio makubwa baada ya kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi 4,133 – wakiwemo wanaume 1,925 na wanawake 2,213.
Kupitia banda lake, Wizara ilitoa elimu kuhusu haki za binadamu, masuala ya katiba, ardhi, ndoa, mirathi, pamoja na kesi za jinai na madai. Mkurugenzi Msaidizi wa Haki za Binadamu, Bi Beatrice Mpembo, ameeleza kuwa ubora wa huduma hizo ndio uliifanya Wizara kuwa mshindi wa kwanza kati ya wizara zote zilizoshiriki.
Mbali na ushindi huo, Wizara ilipata pia zawadi maalum kutoka kwa Winifrida Flower kwa kuthamini huduma bora na ushirikiano waliouonyesha.
🎥 Tazama video hii ujionee namna huduma za msaada wa kisheria zilivyowafikia wananchi kwa ukaribu. Pia fahamu wapi unaweza kupata huduma hizi kila siku katika halmashauri za Dar es Salaam na nchi nzima.
#Sabasaba2025 #WizaraYaKatibaNaSheria #MsaadaWaKisheria #HudumaKwaWananchi #MaoneshoYaBiashara #TuzoYaUshindi #DarEsSalaam.