Skip to main content

KISA CHA MTOTO WA MIAKA 9 ALIYEACHA SHULE NA KUGONGA MAWE.

Submitted by admin on 23 October 2025

Kupitia juhudi za MSLAC kwa ushirikiano na Maafisa Dawati la Jinsia na Watoto wa Wilaya ya Kigamboni, binti wa miaka 9 aitwaye Ashura, mwanafunzi wa darasa la nne, ameweza kurejea shuleni baada ya kuacha masomo kutokana na ugumu wa maisha.

Ashura aliacha shule ili kwenda kugonga mawe na kusaidia bibi na babu yake, lakini kupitia ufuatiliaji na elimu tuliyotoa shuleni, wanafunzi wenzake walitoa taarifa kuhusu hali yake. Timu yetu ilifika nyumbani kwao, tukafanya mazungumzo na walezi wake, na hatimaye tukamrejesha shuleni.

Sasa Ashura anaendelea na masomo, chini ya uangalizi wa Afisa Ustawi wa Jamii wa mtaa wake, kuhakikisha anapata msaada na ufuatiliaji unaohitajika.

🎯 Kisa hiki kinatukumbusha umuhimu wa kushirikiana katika kulinda haki za watoto na kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi ya elimu bora.

#MSLAC #Kigamboni #ElimuKwaWatotoWote #HakiZaWatoto #Ashura #DawatiLaJinsia #UstawiWaJamii #WatotoNaElimu