Mama Samia Legal Aid Campaign
Yaliyojiri
Posted:
#MSLAC inawatakia Wakristo wote Ijumaa Kuu njema! Mungu awape baraka tele, furaha, na amani katika siku hii muhimu ya ibada na kutafakari. Ijumaa Kuu iwe mwanzo wa baraka tele katika maisha yenu. Amani na Upendo katika Haki. #MSLAC #Katibayawatu #Katibanasheria
Posted:
Mahafali ya kwanza ya wahitimu wa kozi ya wasaidizi wa kisheria katika Chuo cha Law School of Tanzania (LST) ni hatua muhimu sana katika maendeleo ya mfumo wa kisheria nchini Tanzania.Kuanza kwa kozi hii kunamaanisha kwamba serikali inatambua umuhimu wa kuwa na wataalamu wengi zaidi katika uwanja…
Posted:
Msaada wa kisheria ni huduma au usaidizi unaotolewa na wataalamu wa sheria kwa watu ambao wanahitaji msaada katika masuala yanayohusiana na sheria. Huduma hii inaweza kujumuisha ushauri wa kisheria, msaada wa kisheria katika kesi za mahakama, mchakato wa kutafuta haki. #MSLAC
Posted:
TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA Taratibu za kuandika wosia zinatofautiana kulingana na sheria ya mirathi inayotumika. 1. WOSIA WA MAANDISHI Wosia huu unashuhudiwa na watu wawili pale ambapo mtoa wosia anajua kusoma au kuandika. Shuhuda mmoja lazima awe ndugu wa karibu wa mtoa wosia na…
Posted:
*MIAKA 3 YA MAFANIKIO KATIKA UDHBITI WA HAKI JINAI*#SisiNdioWajenziWaTanzaniaYetu #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #Sisinitanzania #Matokeochanya #MSLAC #SamiaSuluhuHassan #ChamaChaMapinduzi #Philipmpango
Posted:
MSLAC inatoa ufafanuzi juu ya haki na wajibu wa mtu katika muktadha wa masuala ya kisheria. Ushauri huu unaweza kujumuisha kutathmini hali ya kisheria na kutoa maelezo kuhusu njia za kisheria zinazopatikana. #MSLAC
Posted:
MSLAC inajitahidi kupigania haki za binadamu na kufanya kazi na mashirika mengine ya kiraia na serikali ili kuboresha mfumo wa sheria na kuhakikisha upatikanaji wa haki sawa kwa kila mtu. #MSLAC